11 Juni 2015 - 12:26
Serikali ya Marekani kutuma wanajeshi wengine 450 Iraq

Rais wa Marekani Barack Obama ameidhinisha kutumwa kwa wanajeshi 450 zaidi nchini Iraq kwenda kutoa mafunzo na ushauri wa kijeshi kwa jeshi la Iraq ili liweze kupambana na wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi la kigaidi la Daesh

Rais wa Marekani Barack Obama ameidhinisha kutumwa kwa wanajeshi 450 zaidi nchini Iraq kwenda kutoa mafunzo na ushauri wa kijeshi kwa jeshi la Iraq ili liweze kupambana na wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi la kigaidi la Daesh. Ikulu ya Rais wa Marekani imesema wanajeshi hao watajiunga na kikosi kilichoko tayari Iraq cha wanajeshi 3,100 kulisaidia jeshi la Iraq na pia wapiganaji wa kisunni. Kikosi hicho kipya kitazingatia zaidi operesheni yao katika kuukomboa mji wa Ramadi katika jimbo la Anbar unaodhibitiwa na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh. Obama amefutilia mbali uwezekano wa kuyatuma majeshi ya ardhini nchini Iraq akihofia kufanya hivyo, kutawaingiza wanajeshi wa Marekani katika vita alivyofanya juhudi kubwa kuvimaliza.

Wanajeshi hawa wanaongezwa baada ya kuonekana kuwa wanajeshi wa Marekani waliokuwepo Iraq hakufanikiwa kufikia lengo lao lililowapeleka na hatimaye kusababisha wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh kuzidi kujidhatiti katika miji ya Iraq na kuendelea kufanya mauaji ya kinyama dhidi ya wananchi wa Iraq na Syria.